You are here

Kiswahili

In the media

LVEMP II Project

EA SusWatch is currently implementing the LVEMP II Civil Society Watch Project that seeks to lobby and advocate for realization of results-based performance from the Lake Victoria Environmental Management Project (LVEMP II) and implementation of the East African Climate Change Policy (EACCP, April 2011). Read More about LVEMP II - Click!

Ukurasa wa habari inaeleza kuhusu upungufu wa maji katika bonde la ziwa victoria

Shukrani
Toleo hili shirikishi la Sera ya Mabadiliko ya Tabianchi ya Afrika Mashariki limeandaliwa kwa dhumuni la kuongeza uelewa na kuhamasisha ushiriki mpana wa wananchi, asasi za kiraia na viongozi ngazi ya kitaifa na wale wa vijiji katika bonde la Ziwa Viktoria, ambapo hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi zinahitajika.
Kijitabu hiki ni matokeo ya kazi za watu mbalimbali na mashirika. Shukurani za pekee zimwendee Obed Mahenda na Wallace Mayunga kwa kazi yao ya kuandaa kijitabu hiki, mchoraji katuni Ali Masoud Kipanya kwa michoro yake ya kusisimua, na wafanyakazi wa mtandao wa SusWatch walioko katika ofisi za Mtandao wa Maendeleo Endelevu Uganda (UCSD): Kimbowa Richard, Ken Oluoch, David Mwayafu, Emily Arayo, Rebecca Kwagala, Mtandao wa Sus Watch Kenya: Nobert Nyandire na Henry Ligedere na Mtandao wa Maendeleo Endelevu Tanzania (TCSD) Sam Kasulwa, na Godwin Kalokola kwa ushirikiano wao katika kuandaa kijitabu hiki

 

Utangulizi
Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria Awamu ya II (ambao pia unajulikana kama LVEMP II) ni Mradi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambao unatekelezwa katika nchi tano ambazo zinatumia Bonde la Ziwa Victoria ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.
LVEMP II ni mradi mtambuka mipaka ambao umeanzishwa ili kufanikisha malengo mawili ya kimaendeleo/malengo ya dunia ya kimazingira. Mosi, mradi umeandaliwa ili kuboresha usimamizi shirikishi wa rasilimali mtambuka ya bonde la ziwa Victoria, na pili, kupunguza athari za kimazingira katika ziwa ambazo zinatokana na uchavuzi wa mazingira katika maeneo lengwa pamoja na vyanzo vya maji vilivyokusudiwa (kama vile vyanzo vya maji vya mto Katonga nchini Uganda, Nyando nchini Kenya, Simiyu nchini Tanzania).Yote haya ni kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii ambazo zinategemea rasilimali ya hili Bonde.

 

LVEMP II Mradi wa Asasi Angalizi za Kijamiini mradi wa miaka mitatu chini ya Mtandao Angalizi wa Uendelevu wa Afrika Mashariki ambao unatekelezwa kuanzia mwezi Novemba 2011 hadi mwezi Oktoba 2014, kwa ufadhili wa serikali ya Sweden.
Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa taasisi za Muungano wa Maendeleo Endelevu wa Uganda (UCSD), Muungano wa Maendeleo Endelevu Tanzania (TCSD), na Mtandao Angalizi wa Mazingira Endelevu wa Kenya (SusWatch Kenya).
Sekretarieti ya Kikanda ya mradi wa SusWatch inahifadhiwa na UCSD iliyoko mjini Kampala, Uganda. Mradi huu ambao ulianzishwa mwaka 2005, unalenga kuhamasisha taasisi za jamii katika ukanda wa Afrika Mashariki kusisitiza juu ya uwajibikaji miongoni mwa serikali na taasisi za maendeleo za kimataifa ili kuakikisha dunia endelevu katika maswala ya kijamii na kimazingira.
Mamlaka ya Mradi huu ni kufuatilia na kuhamasisha utekelezaji wa majukumu ya kitaifa na kikanda katika mikataba ya kimataifa na mipango mingineyo kwa ajili ya maendeleo endelevu katika ukanda wa Afrika Mashariki.

AFRIKA MASHARIKI - Waangalizi wa: June - December 2012
 

 

Jarida hili kuhusu utayari juu ya mabadiliko ya tabia nchi limetolewa na Mtandao wa Uangalizi wa Uendelevu wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kuonyesha maendeleo katika utekelezaji wa makubaliano katika sera ya Afrika

 

Mtandao wa Uangalizi wa Uendelevu wa Afrika Mashariki unaendesha mradi unaojulikana kama Waangalizi wa Asasi za Kiraia juu ya LVEMP II ambao unalenga kushawishi juu ya ufanisi katika utekelezaji wa mradi huu wa kanda,miongoni mwa mambo mengine. Jarida hili la nne la Waangalizi wa Uendelevu wa Afrika linalenga zaidi kwenye “Maendeleo ya Mradi wa LVEMP II katika Africa Mashariki”.

 

The East African Sustainability (SusWatch) Network is a network of NGOs from Kenya, Uganda and Tanzania spearheaded by Uganda Coalition for Sustainable Development (UCSD), Sustainable Environmental Development Watch Network (SusWatch Kenya), and Tanzania Coalition for Sustainable Development (TCSD). EA SusWatch Regional Secretariat is hosted by UCSD in Kampala, Uganda.

Read more

With Support From

Partners